Ibn ´Uthaymiyn kutanguliza mikono katika Sujuud

Kusujudu kwa kuanza magoti ndio bora zaidi kisha ndio mtu afuatishe mikono, paji la uso na pua. Mtu asianze kusujudu kwa mikono. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza hilo pale aliposema:

“Mmoja wenu anapoenda katika Sujuud, asishuke kama anavoshuka ngamia.”[1]

Ngamia huanza kwenda chini kwa mikono kama jinsi imevyoshuhudiwa. Kila anayemuona ngamia anapoenda chini ameona kuwa anatanguliza mikono kwanza. Hivyo usitangulizwe mikono. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza hilo. Binadamu kujifananisha na wanyama, khaswa katika swalah, ni jambo lisilotakikana.

[1]Abu Daawuud (840).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/395)
  • Imechapishwa: 31/05/2023