Ni wajibu kusoma al-Faatihah kwa kusimama

Ni wajibu kusoma al-Faatihah hali ya kuwa mtu amesimama. Kuhusiana na yale yanayofanywa na baadhi ya watu pindi anaposimama imamu ili kuswali Rak’ah ya pili kwa mfano, wamuona anakaa na kusoma al-Faatihah na anasimama pamoja na imamu baada ya kuwa kishasoma nusu ya al-Faatihah. Tunamwambia mtu huyu kisomo chako cha al-Faatihah sio sahihi. Kwa kuwa ni wajibu kusoma al-Faatihah katika hali ya kusimama. Kisomo chako hichi hakisihi kwa kuwa umesoma baadhi yake kwa kukaa, ilihali wewe ni muweza wa kusoma kwa kusimama.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/391)
  • Imechapishwa: 31/05/2023