10. Walinganizi kukabiliana na upotoshaji unaosambazwa

Kwa kuzingatia kuenea kwa ulinganizi kwa mujibu wa misingi haribifu, ukafiri, ukanaji wa Mola wa waja, ukanushaji wa Ujumbe, ukanushaji wa Aakhirah, kuenea kwa ulinganizi wa ukristo katika nchi nyingi na madai mengine mengi, basi kulingania kwa Allaah hii leo imekuwa ni faradhi yenye kuenea, lazima kwa wanazuoni wote na kwa watawala wote ambao wanaamini dini ya Uislamu. Ni lazima kwao kufikisha dini ya Allaah kulingana na uwezo wao kwa njia ya maandishi, mazungumzo, kwa njia ya redio na kwa kila njia wanayoweza. Wasishindwe kufanya hivo au wakamtegemea huyu na yule. Haja na dharurah hii leo ya kusaidiana na kushirikiana imekuwa kubwa. Kusaidiana juu ya jambo hili kubwa kunatakiwa kuwe kukubwa kushinda hapo kabla. Maadui wa Allaah wamesaidiana kwa kutumia kila njia ya kuwazuia watu kutokamana na njia ya Allaah, kuitilia shaka dini Yake na kuwaita watu katika mambo yanayowatoa nje ya dini ya Allaah (´Azza wa Jall). Kwa hivyo ni lazima kwa waislamuwakabiliane na uchangamfu huu unaopotosha na uchangamfu wa kikafiri kwa uchangamfu wa kiislamu na ulinganizi wa kiislamu kwa ngazi mbalimbali, kwa kila njia na kwa njia zote zinazowezekana. Hili ni kwa njia ya kutekeleza yale ambayo Allaah amewawajibishia waja Wake katika kulingania katika njia Yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Da´wah ilaa Allaah wa Akhlaaq-id-Du´aah, uk. 19-20
  • Imechapishwa: 31/05/2023