Kwa nisba ya watawala na kwa wale ambao wana uwezo mpana wanao wajibu mkubwa zaidi na wanalazimika kufikisha ulinganizi katika zile pembe zote za nchi kiasi cha wanavoweza. Wafanyehivokulingana na uwezo kwa zile njia zinazowezekana na kwa zile lugha hai zinazoongewa na watu. Ni lazima wafikishe amri ya Allaah kwa lugha hizo mpaka dini ya Allaah iweze kumfikia kila mmoja kwa lugha anayoijua ni mamoja ya kiarabu au nyingine. Jambo hivi sasa limekuwa lenye kuwezekana na jepesi kwa njia ambazo tumetangulia kuzitaja; redio, runinga, vyombo vya mawasiliano na nyinginezo ambazo ni rahisi hii leo na hazikuwa rahisihapo kale.

Ni lazima vilevile kwa wahubiri katika sherehe, mikusanyiko na sehemu nyinginezo wafikishe kile wanachokiweza katika amri ya Allaah (´Azza wa Jall) na waitawanye dini ya Allaah kwa kiasi cha uwezo na elimu yao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Da´wah ilaa Allaah wa Akhlaaq-id-Du´aah, uk. 18
  • Imechapishwa: 31/05/2023