Ibn ´Uthaymiyn kuhusu katuni za mafunzo kwa watoto

Swali: Kuna kanda za video zilizo na mapicha zinazofanya harakati za wanyama au vitu vyenginevyo zinazosimulia visa vya kimalezi vya kihistoria zisizokuwa na nyimbo wala muziki. Ni ipi hukumu ya kanda hizi? Unasemaje juu ya wale wanaotazama visa vya watoto vya uongo ambavyo ambavyo vinahimiza katika maadili ya Kiislamu?

Jibu: Picha hizi zinazofanya harakati ni picha ambazo ziko kwa ishkali ya kutisha ambazo kunakhofiwa juu ya akili ya mtoto au hapana? Ikiwa ni hilo la mwanzo basi hazifai. Kwa sababu ni lazima kuwaepusha watoto wetu na kila kitu kinachoshawishi akili zao.

Ama ikiwa ni picha zenye kuingia akilini na kuna mafunzo ndani yake hazina neno. Kwa sharti mtu asiegemeze kisa kwa mtu maalum ambaye hakufanya hivo. Wanachuoni (Rahimahumu Allaah) mpaka hii leo ni wenye kuendelea kupiga mifano kwa kusema “kama mtu akifanya kadhaa” lakini si ukweli wa mambo. Wanachokusudia ni kuleta picha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (74) http://binothaimeen.net/content/1720
  • Imechapishwa: 20/08/2020