Swali: Sisi ni wanafunzi katika Chuo kikuu Saudia na kuna Raafidhwah wengi. Kishari´ah vipi tutaamiliana nao?
Jibu: Amiliana nao kama jinsi wanavyoamiliana nawe. Na walinganie katika haki. Kila mtu wa Bid´ah amiliana naye kama jinsi anavyoamiliana nawe na mlinganie katika haki. Wengi katika wafuasi wa viongozi wa Ahl-ul-Bid´ah hawajui kuwa wamo katika Bid´ah. Wanawajengea dhana nzuri watu wanaowafuata bila ya kujua. Lau unajadiliana nao kwa uzuri na ukawabainishia haki wanarejea [katika haki]. Hivyo yatakiwa kutofautisha baina ya mwenye kulingania katika Bid´ah na baina ya mfuata kichwa mchunga asiyejua kitu. Kwa vyovyote tunaamiliana nao kama jinsi wanavyoamiliana nasi; lakini twatakiwa kuwalingania katika haki na kuwabainishia upotofu waliomo wa Bid´ah na huenda Allaah Akawaongoza.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (201 B)
- Imechapishwa: 09/04/2022
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)