06. Ni ipi tofauti kati ya swalah ya Tarawiyh, kisimamo cha usiku na Tahajjud?

Swali: Ni ipi tofauti kati ya swalah ya Tarawiyh, kisimamo cha usiku na Tahajjud?

Jibu: Swalah ya usiku inaitwa Tahajjud na inaitwa kisimamo cha usiku. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ

“Amka sehemu ya usiku na uswali ni ziada ya sunnah kwako.”

يَا أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ قُمِ اللَّيْلَ إِلَّا قَلِيلًا

“Ee uliyejifunika! Simama usiku [uswali] kucha isipokuwa [muda] mdogo tu.”[1]

Amesema (Subhaanah) katika Suurah ”adh-Dhaariyaat” kuhusu waja Wake wenye kumcha:

آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُحْسِنِينَ كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ

”Wakichukua yale atakayowapa Mola wao. Hakika wao kabla ya hapo walikuwa ni wahisani. Walikuwa wakilala kidogo tu usiku.”[2]

Kuhusu Tarawiyh wanazuoni husema hivo kwa kuachia na wakakusudia kisimamo cha usiku katika Ramadhaan mwanzoni mwa usiku pamoja na kuchunga jambo la kuwepesisha na kutorefusha. Vilevile inafaa kuiita Tahajjud na kuiita kisimamo cha usiku na wala hakuna magomvi katika jambo hilo.

[1] 73:01

[2] 51:16-17

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Swalaat-it-Taraawiyh, uk. 10
  • Imechapishwa: 09/04/2022