05. Hukumu ya du´aa ya kukhitimisha Qur-aan

Swali 38: Unasemaje juu ya yale wanayoonelea baadhi ya watu kwamba du´aa ya kukhitimisha Qur-aan ni miongoni mwa Bid´ah zilizozuliwa?

Jibu: Sijui du´aa ya kukhitimisha Qur-aan ndani ya swalah msingi sahihi ambao kwao mtu anaweza kutegemea juu yake kutoka katika Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala kutoka katika matendo ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Kubwa linalopatikana katika hayo ni yale yaliyokuwa yakifanywa na Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) anapotaka kumaliza Qur-aan basi alikuwa akiwakusanya familia yake na akiomba du´aa[1]. Lakini haya ni nje ya swalah.

Zaidi ya hayo, ukhitimishaji huu – licha ya kwamba hakukuthibiti na hakuna msingi kutoka katika Sunnah – ni kwamba watu, khaswa wanawake, wanakuwa wengi katika msikiti huu maalum na hivyo matokeo yake kunatokea mchanganyiko kati ya wanawake na wanamme wakati wanapotoka nje ya msikiti, jambo ambalo linatambulika kwa wale wenye kuliona.

Lakini baadhi ya wanazuoni wamesema kuwa inapendekeza kukhitimisha Qur-aan kwa du´aa hii.

Na lau imamu atafanya du´aa hii ya kukhitimisha katika kisimamo cha mwisho wa usiku na akasoma mahali pake du´aa ya Qunuut katika Witr ni sawa. Kwa sababu Qunuut imewekwa katika Shari´ah.

[1] ad-Daarimiy (02/468).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Swalaat-it-Taraawiyh, uk. 09-10
  • Imechapishwa: 09/04/2022