Ibn Taymiyyah kuhusu anayetaka kuswali ´Aswr wakati wa Maghrib

Swali: Katika “Majmuu´-ul-Fataawaa” Shaykh-ul-Islaam aliulizwa kuhusu mtu ambaye amekosa swalah ya ´Aswr ambapo baadaye akaja msikitini na kukuta kunaswaliwa swalah ya Maghrib. Je, aswali ile swalah aliyokosa kabla ya Maghrib au hapana? Akajibu (Rahimahu Allaah) kwamba anatakiwa kuswali Maghrib pamoja na imamu kisha ndio aswali ´Aswr kwa makubaliano ya wanazuoni. Halafu akataja (Rahimahu Allaah) makinzano ya wanazuoni kuhusu kuirudia Maghrib baada ya kuswali ´Aswr. Je, jawabu lake Shaykh-ul-Islaam ni sahihi au si sahihi?

Jibu: Makusudio yake ni kwamba aswali pamoja nao Maghrib swalah inayopendeza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kunapokimiwa swalah na wewe uko msikitini basi swali pamoja nao.”

Usiseme kuwa umeshaswali na hivyo siswali. Kwa hivyo swali pamoja nao. Baadhi ya wanazuoni wamesema kuwa inasihi ingawa ameitanguliza mbele ya ´Aswr. Baadhi ya wengine wamekataa na kwamba anaiswali kama swalah ya Sunnah. Kwa msemo mwingine asiketi chini ilihali watu wanaswali. Baada ya hapo ndio aswali Maghrib baada ya kuswali ´Aswr ili kupatikane suala la kupangilia, jambo ambalo ndio sahihi. Aswali ´Aswr kisha baadaye ndio aswali Maghrib. Ukifika wakati wa Maghrib ataswali pamoja nao swalah inayopendeza ili asiketi chini na huku watu wanaswali. Na ikiwa ataiswali [Maghrib] kwa nia ya ´Aswr kisha akazidisha Rak´ah nyingine moja maoni yaliyo dhahiri ni kwamba inasihi. Nia haiathiri kitu muda wa kuwa amekamilisha kwa upande wa kitendo chenyewe.

Jambo la wajibu ni yeye kuswali pamoja nao swalah ya Sunnah kisha akaswali ´Aswr na baada ya hapo akaswali Maghrib, kwa sababu Allaah ameipangilia namna hii. Ni sawa pia akiswali ´Aswr peke yake kisha akajiunga nao katika Maghrib.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23450/حكم-من-فاتته-صلاة-العصر-واقيمت-المغرب
  • Imechapishwa: 30/01/2024