Kusikiliza Qur-aan kwa lengo la kutafuta ponyo

Swali: Kuna mwanamke mgonjwa anayeweka karibu na kichwa chake redio ikisoma Qur-aan na akapona. Je, inafaa kuitakidi kuwa Qur-aan ndio imemponyesha? Je, kitendo hichi kinajuzu?

Jibu: Hapana. Hii maana yake ni kwamba anapata raha kwa kusikiliza Qur-aan. Kuna uwezekano kupata kwake raha ni kwa kule kusikiliza kwake Qur-aan na kufurahi kwake ni miongoni mwa sababu zinazomridhisha Allaah na sababu za kupona kwake. Vinginevyo ponyo si kutokana na Qur-aan. Ponyo ni kutokana na Allaah (Jalla wa ´Alaa). Lakini Allaah ameifanya Qur-aan kuwa ni ponyo, kwa sababu ni maneno Yake (Subhaanah):

قُلْ هُوَ لِلَّذِينَ آمَنُوا هُدًى وَشِفَاءٌ

“Sema: “Hiyo ni kwa walioamini ni mwongozo na shifaa.””[1]

Mtu anapata ladha kwayo, anaisoma na anajitibu kwayo. Aidha aitakidi kuwa Allaah ameifanya kuwa ni ponyo. Ponyo inatokana na Allaah, na si kutokana na maneno yenyewe. Ponyo ni kutokana na Allaah. Hata hivyo Allaah amefanya kuizingatia Qur-aan, kumsomea nayo mgonjwa na kumsomea du´aa nzuri mgonjwa ni miongoni mwa sababu za kupona.

[1] 41:44

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23452/حكم-سماع-القران-من-المذياع-بغرض-الشفاء
  • Imechapishwa: 30/01/2024