395 – ´Uqbah bin ´Aamir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Tulikuwa pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tulikuwa tunamuhudumia wenyewe na tunawachunga ngamia wetu kwa kupokezana. Wakati ilipokuwa zamu yangu, basi nikawatoa wakati wa asubuhi ambapo nikamuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesimama akisema:

ما مِنكم مِن أحدِ يتوّضأُ فيُحسِنُ الوضوءَ، ثمّ يقوم فيركع ركعتين يُقبلُ عليهما بقلبِه ووجهه؛ إلا قد أوجَبَ . فقلتُ: بخٍ بخٍ! ما أجودَ هذه

“Hakuna yeyote katika nyinyi atakayetawadha akatia vizuri wudhuu´ wake kisha akasimama na kuswali Rak´ah mbili, akaziuelekezea moyo wake na uso wake, isipokuwa itamthubutukia.” Ndipo nikasema: “Bishara, bishara! Ni ukarimu uliyoje huu!”[1]

Ameipokea Muslim, Abu Daawuud, na tamko ni lake, an-Nasaa’iy, Ibn Maajah, Ibn Khuzaymah na al-Haakim, isipokuwa kwake imekuja:

ما مِن مسلم يتوضأ فيُسبغُ الوضوءَ ثم يقوم في صلاته، فيعلمُ ما يقول؛ إلاَّ انفتل وهو كيومَ ولدته أُمه

“Hakuna muislamu yeyote atakayetawadha na akaeneza vizuri wudhuu´ kisha akasimama katika swalah yake na huku akieleza kile anachokisema, isipokuwa ataimaliza akiwa msafi kama ile siku aliyozaliwa na mama yake.”[2]

Halafu akasema:

“Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh.”

Kumthubutukia maana yake ni kwamba amefanya yale yanayomthubutukia yeye kuingia Peponi.”

[1] Swahiyh.

[2] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/282-283)
  • Imechapishwa: 30/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy