69. Hadiyth ”Hakika tumejua namna ya kukutakia amani… ”

69 – ´Aliy bin ´Abdillaah ametuhadithia: Marwaan bin Mu´aawiyah ametuhadithia: ´Uthmaan bin Hakiym ametuhadithia: Khaalid bin Salamah ametuhadithia, kutoka kwa Muusa bin Twalhah: Zayd bin Khaarijah – Nduguye Banuul-Haarith bin al-Khazraj – amenikhabarisha:

”Nilisema: ”Ee Mtume wa Allaah! Hakika tumejua namna ya kukutakia amani, tunakuswalia namna gani?” Akasema: ”Niswalieni na semeni:

اللهم بارك على محمد و على آل محمد، كما باركت على إبراهيم و آل إبراهيم، إنك حميد مجيد

”Ee Allaah! Mbariki Muhammad, jamaa zake Muhammad kama Ulivyombariki  na Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. Ameipokea an-Nasaa´iy kwa mukhtaswari: Sa´iyd bin Yahyaa bin Sa´iyd al-Umawiy ametukhabarisha, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Uthmaan bin Hakiym, kutoka kwa Muusa bin Twalhah, ambaye amesema:

”Nilimuuliza Zayd bin Khaarijah, mimi nilimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akasema: ”Niswalieni, jitahidini katika du´aa na semeni:

اللهم صل على محمد و على آل محمد

”Ee Allaah! Msifu Muhammad na jamaa zake Muhammad.”

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 65-66
  • Imechapishwa: 30/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy