68 – ´Aliy bin ´Abdillaah ametuhadithia: Muhammad bin Bishr ametuhadithia: Mujammiy´ bin Yahyaa ametuhadithia, kutoka kwa ´Uthmaan bin Mawhib, kutoka kwa Muusa bin Twalhah – pengine kutoka kwa baba yake, kitu ambacho hakipo kwenye kitabu changu – ambaye amesema:

”Nilisema: ”Ee Mtume wa Allaah! Ni vipi kukuswalia? Akasema: ”Semeni:

اللهم صل على محمد كما صليت على إبراهيم,إنك حميد مجيد. و بارك على محمد و على آل محمد كما باركت على إبراهيم,إنك حميد مجيد

”Ee Allaah! Msifu Muhammad kama Ulivyomsifu Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa. Na mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad kama Ulivyombariki Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. Wanamme wake ni wanamme wa Swahiyh. Imaam (1/162) ameipokea kupitia kwa Muhammad bin Bishr. an-Nasaa´iy ameipokea kupitia njia nyingine kutoka kwa Muhamamd bin Bishr.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 64-65
  • Imechapishwa: 30/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy