67. Hadiyth ” Tunajua kukutakia amani, ni namna gani ya kukuswalia… ”

67 – Ibraahiym bin Hamzah ametuhadithia: ´Abdul-´Aziyz bin Abiy Haazim na ´Abdul-´Aziyz bin Muhammad wametuhadithia, kutoka kwa Yaziyd, kutoka kwa ´Abdullaah bin Khabbaab, kutoka kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy, ambaye amesema:

”Tulisema: ”Ee Mtume wa Allaah! Tunajua kukutakia amani, ni namna gani ya kukuswalia?” Akasema: ”Semeni:

اللهم صل على محمد عبدك و رسولك، كما صليت على إبراهيم، و بارك علىى محمد و على آل محمد، كما باركت على إبراهيم و على آل إبراهيم

”Ee Allaah! Msifu Muhammad, mja na Mtume wako, kama Ulivyomsifu Ibraahiym. Na mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad kama Ulivyombariki Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy.  Ibraahiym bin Hamzah ni Abu Ishaaq Ibraahiym bin Muhammad bin Hamzah al-Madaniy. al-Bukhaariy ameipokea Hadiyth katika ”as-Swahiyh” kupitia cheni ya wapokezi ya mtunzi.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 64
  • Imechapishwa: 30/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy