Swali: Baadhi ya wanafunzi wanachukua minyororo ya wapokezi ya al-Bukhaariy na Muslim kwa ajili ya kuzisoma na kuzikosoa. Wanasema kwa mfano wanapotaja cheni ya al-Bukhaariy ya kwamba Hadiyth hii ni nzuri. Vivyo hivyo kuhusu Muslim.
Jibu: Maimamu wameafikina juu ya kuzikubali Hadiyth za ndani ya al-Bukhaariy na Muslim. Isipokuwa mambo machache ambayo al-Daraaqutwniy ameyakosoa ndani ya Muslim. Vinginevyo maimamu wameafikiana juu ya kukubali mapokezi ya al-Bukhaariy na Muslim na kwamba baada ya kuzidurusu na kuzipatiliza imebainika kusalimika kwake upande wa cheni zake. Watunzi wawili, al-Bukhaariy na Muslim, wamejitahidi katika hilo na kuzichagua kutoka katika mkusanyiko wa Hadiyth nyingi. Allaah awarehemu. Cheni zake ziko wazi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24617/هل-يوجد-خلاف-في-قبول-البخاري-ومسلم
- Imechapishwa: 14/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
94. Pindi watu watalazimika kuzikana usiku
92- Watu wakilazimika kuzika wakati wa usiku itafaa ijapo ni kwa kutumia mataa na kushuka nayo ndani ya kaburi. Yote hayo kwa ajili ya kuwepesisha zoezi la mazishi. Dalili ni Hadiyth ya Ibn ´Abbaas aliyesimulia: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwingiza mtu mmoja ndani ya kaburi lake…
In "14. Mlango wa kumi na nne: Uzikaji na yanayofuatilia hilo"
16. Maafikiano ya ummah juu ya al-Bukhaariy na Muslim
Sehemu kubwa ya Hadiyth zilizopo kwa al-Bukhaariy na Muslim kuna uhakika ya kwamba yamesemwa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam). Mosi ni kwamba kiasi kikubwa kilichotajwa kinakuwa sampuli hiyo na pili ni kwamba wanazuoni wamezipokea kwa ridhaa na kuzisadikisha. Jengine ni kwamba ummah mzima hauwezi kukubaliana juu ya kosa.…
In "Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr"
02. Hadiyth Swahiyh kuhusu uharamu wa picha
al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Allaah (Ta´ala) amesema: “Ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule ambaye anajaribu kuumba mfano wa viumbe Wangu? Hebu waumbe mdudu chungu, waumbe punje ya nafaka au waumbe chembe…
In "al-Jawaab al-Mufiyd fiy Hukm-it-Taswwiyr"