92- Watu wakilazimika kuzika wakati wa usiku itafaa ijapo ni kwa kutumia mataa na kushuka nayo ndani ya kaburi. Yote hayo kwa ajili ya kuwepesisha zoezi la mazishi. Dalili ni Hadiyth ya Ibn ´Abbaas aliyesimulia:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwingiza mtu mmoja ndani ya kaburi lake usiku na akawasha taa ndani ya kaburi lake.”

Ameipokea Ibn Maajah (01/464), at-Tirmidhiy (02/157) kwa ukamilifu zaidi na akasema:

“Hadiyth ni nzuri.”

Bi maana ni nzuri kupitia zengine. Istilahi hii ni maalum kwa at-Tirmidhiy pindi anaposema:

“Hadiyth ni nzuri.”

basi anakusudia kuwa ni nzuri kupitia zengine. Yeye mwenyewe ndiye amesema hivo katika “al-´Ilal” yaliyotajwa mwishoni mwa kitabu chake. Imepokelewa shahidi yake kama itavyokuja. Kutokana na hayo ukosoaji wa Ibn-ul-Qattwaan uliyotajwa na mtunzi wa “Tuhfat-ul-Ahuudhiy” juu ya at-Tirmidhiy kuifanya kuwa nzuri hauna maana yoyote.”

Kuhusu shahidi ni kutoka katika Hadiyth ya Jaabir bin ´Abdillaah:

Ameipokea Abu Daawuud (02/63), al-Haakim (01/367) na al-Bayhaqiy (04/53). al-Haakim amesema:

“Swahiyh juu ya sharti za Muslim.” adh-Dhahabiy ameafikiana naye. an-Nawawiy amezidisha juu yake na akasema katika “al-Majmuu´” (05/302):

“Ameipokea Abu Daawuud kwa cheni ya wapokezi juu ya sharti za al-Bukhaariy na Muslim.”

Yote hayo ni makosa. Mzunguko wa cheni ya wapokezi wake ni kwa Muhamamd bin Muslim at-Twaa-iy. Mtu huyu, ijapo ni mwaminifu yeye kama yeye, lakini alikuwa mnyonge katika hifdhi yake. Ndio maana al-Bukhaariy na Muslim hawakumtumia kama hoja. al-Bukhaariy amemtolea hali ya kumwekea taaliki na Muslim hali ya kuegemea kwa zengine ambazo ni Swahiyh. Miongoni mwa mambo ya kushangaza ni kwamba al-Haakim na adh-Dhahabiy ni watambuzi juu ya baadhi ya mambo haya. al-Mizziy ametaja kwamba at-Twaa-iy huyu hana katika Muslim isipokuwa Hadiyth moja pekee. al-Haafidhw Ibn Hajar amesema: “Ni mwenye kumfuata kwake, kama alivosema hayo al-Haakim.” Kadhalika adh-Dhahabiy amesema kwa uwazi katika kichwa cha khabari yake kutoka katika “al-Miyzaan” kwamba Muslim amemtolea hali ya kumfuata.

Pia inayo shahidi nyingine kutoka katika Hadiyth ya Abu Dharr mfano wake.

Ameipokea al-Haakim kwa cheni ya wapokezi ambayo yupo bwana mmoja ambaye hakutajwa kwa jina. Wapokezi wake wengine waliobaki ni waaminifu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 180-181
  • Imechapishwa: 21/02/2022