Hukumu ya umanjano na uchafuchafu kabla na baada ya hedhi

Swali: Tunataraji utatuwekea uwazi maoni yenu juu ya manjano na uchafu kabla na baada ya hedhi. Kuna mwanamke anasema kuwa hedhi yake ni lazima itanguliwe na uchafu au umanjano. Baadhi ya wanawake wanasema kuwa siku zote karibu na hedhi ni lazima kwanza wapate uchafuchafu kwa sifa ya kuendelea. Tunataraji utatuwekea wazi hayo kwa upambanuzi.

Jibu: Naona kuwa umanjano kabla ya hedhi si chochote, kwamba umanjano baada ya hedhi si chochote na kwamba umanjano katikati ya hedhi ni kitu. Kwa sababu katika hali hii bado hajatwaharika.

Kwa mfano mwanamke amezowea kupata ada yake kwa siku tano. Ameona damu katika zile siku mbili za kwanza. Siku ya tatu akaona umanjano. Lakini siku ya nne na ya tano akaona damu. Umanjano huu ulio katikati ya damu mbili unazingatiwa kuwa ni hedhi. Lakini akiona umanjano kwa muda wa siku mbili, tatu au zaidi ya hapo kisha akajiwa na hedhi umanjano huu si chochote. Au akatwahirika na masiku yake yakaisha kisha baada ya hapo akaona umanjano, si chochote. Kwa hivyo umanjano ima ukawa kabla ya hedhi, baada ya hedhi au katikati ya hedhi. Umanjano unaozingatiwa kuwa ni hedhi ni ule unaokuwa katikati ya hedhi pekee.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (66) http://binothaimeen.net/content/1485
  • Imechapishwa: 31/01/2020