Hukumu ya swalah ya mwanamke miguu wazi

Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ya mwanamke ilihali miguu yake iko wazi au amevaa soksi khafifu ambazo zinaonesha sehemu ya mwili?

Jibu: Swalah yake ni batili. Hii ndio fatwa ya wanachuoni tangu wakati wa Shaykh Ibn Baaz na Shaykh al-Albaaniy (Rahimahumu Allaah) kama ilivyo katika al-Fataawaa al-Imaraatiyyah. Amesema kuwa swalah ya mwanamke ni batili ikiwa ataswali na miguu yake iko wazi au sehemu ya chini ya miguu ikionekana wakati wa kusujudu. Katika hali hii swalah yake ibatilika.

Ni lazima kwa mwanamke wakati wa kuswali afunike mwili wake wote isipokuwa uso na viganja vya mikono. Akiwa mbele ya wanaume ambao sio Mahram zake anatakiwa kufunika hata uso na viganja vyake vya mikono.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wusswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.com/index.php?article_id=2697
  • Imechapishwa: 03/05/2015