Si lazima kufunga siku sita za Shawwaal kwa kufuatanisha

Swali: Mimi nafunga siku sita za Shawwaal lakini sifuatanishi masiku. Je, kuna ubaya kwa kufanya hivo?

Jibu: Haina neno ukifunga kwa kufuatanisha au kwa kuachanisha masiku swawm ya Shawwaal. Kwa kuwa Hadiyth imekuja kwa ujumla:

“… na akaifuatanisha na siku sita za Shawwaal.”

Hakusema kwa kufuatanisha. Jambo hili ni sahali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/%205843
  • Imechapishwa: 03/05/2015