Hukumu ya kutamka nia ya kutawadha

Swali: Nikinuia ndani ya msikiti kwa kusema kwa mfano:

اللهم إني نويت الوضوء لصلاة العصر

“Ee Allaah! Hakika mimi nanuia wudhuu´ kwa ajili ya kuswali swalah ya ´Aswr.”

 au nikanuia kuswali kwa njia kama hii – je, kunazingatiwa ni Bid´ah?

Jibu: Kutamka nia, si ndani ya swalah wala katika wudhuu´,  jambo lililowekwa katika Shari´ah. Kwa sababu nia mahali pake ni moyoni. Mtu anakuja kuswali akiwa tayari na nia na inatosha na anasimama kuswali akiwa na nia ya kutawadha na inatosha. Hakuna haja ya yeye kusema kuwa amenuia kutawadha, amenuia kuswali, amenuia kufunga na mfano wa hivo. Nia mahali pake ni moyoni. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika si venginevyo matendo yanategemea na nia na kila mmoja atalipwa kwa kile alichonuia.”

Yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala Maswahabah zake hawakuwa ni wenye kutamka nia ya swalah wala nia ya wudhuu´. Kwa hiyo ni lazima kwetu kuwaigiliza katika hilo na wala tusizue katika dini yetu yale ambayo hayakuidhinisha Allaah wala Mtume Wake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu kitarudishwa.”

Atarudishiwa mwenye nacho.

Kwa haya inapata kutambulika kwamba kutamka nia ni Bid´ah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/423)
  • Imechapishwa: 08/10/2021