Swali: Tunaomba mwongozo juu ya sauti za simu zinazofanana na muziki?

Jibu: Ndugu wanatakiwa kuchunga simu zao zilizo na sauti zinazofanana na sauti za muziki. Ni lazima kubadilisha sauti hizi. Mtu anapasa kufunga simu yake anapoingia msikitini kwa ajili ya kuswali au darsa ili asiwashughulishe watu. Wanafunzi hawatakiwi kujifananisha na watenda madhambi. Hapana haja ya sauti hizo. Weka sauti ya kawaida.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (22)
  • Imechapishwa: 08/10/2021