Kusikiliza Khutbah ya ijumaa kwenye redio kisha anaswali

Swali: Je, inafaa kwangu kusikiliza Khutbah kupitia redio kisha niswali swalah ya ijumaa?

Jibu: Ni lazima kuhudhuria msikitini na usikilize Khutbah kutoka kwa imamu halafu uswali pamoja nao. Lakini huna ijumaa ikiwa uko jangwani au safarini. Badala yake unatakiwa uswali Dhuhr. Lakini sikiliza Khutbah kupitia redio kwa ajili ya kupata faida.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (22)
  • Imechapishwa: 08/10/2021