Hakuna haja ya kutamka nia kwa sauti wakati wa kutawadha

Swali: Ni ipi hukumu ya kutamka nia katika swalah na katika wudhuu´?

Jibu: Hukumu ya hilo ni kwamba ni Bid´ah. Kwa sababu haikunakiliwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala kutoka kwa Maswahabah zake. Kwa hiyo ni lazima kuliacha. Nia mahali pake ni moyoni. Kwa hivyo hakuna haja kabisa ya kutamka nia kwa sauti.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/424)
  • Imechapishwa: 08/10/2021