Swali: Je, nia ni sharti ya kujuzu kukusanya? Inatokea mara nyingi wanaswali Maghrib pasi na nia na baada ya swalah ya Maghrib watu msikitini wanashauriana na hivyo wanaona kukusanya kisha wanaswali ´Ishaa?

Jibu: Nia sio sharti wakati wa ufunguzi wa swalah ya mwanzo. Bali inafaa kukusanya baada ya kumaliza ile ya kwanza kukipatikana sharti yake ambayo ni khofu, ugonjwa au mvua.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/425)
  • Imechapishwa: 08/10/2021