Swali: Mwanamke anapata dhambi ikiwa Hijaab yake inawafitinisha wanamme?

Jibu: Kwa hali yoyote mambo ni kama alivosema Allaah:

وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ

”… na wala msijishauwe kwa kuonyesha mapambo kama walivyojishauwa mwanzo zama za ujahili.”[1]

Mwanamke ameamrishwa kujisitiri, ameamrishwa kutojipamba na kuonyesha mapambo ambayo kunafitinisha. Ni lazima kwake kuvaa mavazi ya kawaida na asiwatie mtihani wanamme.

Swali: Hivi sasa wanatengeneza ´Abaa´ah na wanaandika juu yake jina la mwanamke.

Jibu: Hili ni kosa. Kitendo hicho kinafanya watu kumtazama na ni fitina.

Swali: Ni katika kutambulika?

Jibu: Haifai kufanya hivo. Ni fitina. Haijuzu. Hiyo maana yake ni kwamba anawatambulisha watu ambao wanapita kando naye.

[1] 33:33

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21927/ما-حكم-الحجاب-الذي-فيه-فتنة-للرجال
  • Imechapishwa: 05/10/2022