Swali: Wako wanazuoni wanaosema kuwa uso wa mwanamke sio uchi.

Jibu: Haya ni maoni dhaifu na ni kosa.

Swali: Wanajengea hoja kwa baadhi ya Hadiyth.

Jibu: Hapana. Hadiyth inayosema mwanamke asivae Niqaab ni katika Ihraam. Wakati wa Ihraam hatakiwi kuvaa Niqaab na akavaa Niqaab inayoonyesha macho mawili. Hata hivyo anatakiwa kufunika uso wake kwa kisichokuwa Niqaab. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Wapanda farasi wanaume walikuwa wakitupitia na sisi tuko kwenye Ihraam pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanapotujongelea, kila mmoja wetu anateremsha mavazi yake ya juu, Jilbaab, usoni mwake. Wanapokuwa wameshapita, tunajifunua tena.”[1]

Mwanamke amekatazwa kujisitiri kwa al-Burqu´ ambayo inaonyesha macho mawili peke yake. Jina lake lingine ni Niqaab. Hata hivyo hapana neno kujisitiri kwa isiyokuwa hiyo. Ni kama ambavyo mwanamke amekatazwa kuweka mikononi mwake vifuniko vya mikono. Lakini anatakiwa kufunika mikono yake kwa kitu kingine kisichokuwa vifuniko vya mikono. Inafaa akaifunika kwa ´Abaa´ah au jilbaab. Mwanamme pia amekatazwa kufunika mwili wake kwa kanzu au shati. Anatakiwa kufunika mwili wake kwa shuka ya juu na shuka ya chini. Haifai akaufunika kwa kanzu au shari wala kwa suruwali.

[1] Abu Daawuud.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21924/ما-حكم-القول-بان-وجه-المراة-ليس-بعورة
  • Imechapishwa: 05/10/2022