2 – Majina ya Allaah. Chini ya kanuni hii kuna vipengele vifuatavyo:

1 – Kipengele cha kwanza: Majina yote ya Allaah ni mazuri. Kwa msemo mwingine yamefikia upeo wa uzuri. Yamebeba sifa kamili ambazo hazina upungufu kwa njia yoyote. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلِلّهِ الأَسْمَاء الْحُسْنَى

”Allaah ana majina mazuri mno.”[1]

Mfano wa hilo ni Mwingi wa huruma (الرحمن). Ni moja katika majina ya Allaah (Ta´ala). Jina hilo limejulisha sifa kuu ambayo ni rehema ilionea. Hivyo tunapata kujua kuwa zama الدهر) sio katika majina ya Allaah. Kwa sababu halikubeba maana inayofikia upeo wa uzuri. Kuhusu maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Msitukane zama. Kwani hakika Allaah ndiye zama.”[2]

Maana yake ni kuwa Yeye ndiye mfalme wa zama anayeziendesha. Dalili ya hilo ni maneno yake katika upokezi mwingine kwamba Allaah (Ta´ala) amesema:

”Amri iko mikononi Mwangu. Nageuza usiku na mchana.”[3]

[1] 07:180

[2] Muslim (2246). Ibn Hajar (Rahimahu Allaah) amesema:

”Ameipokea pia Ahmad kwa muundo mwingine kutoka kwa Abu Hurayrah kwa tamko lisemalo: ”Msitukane zama. Allaah amesema: ”Hakika mimi ndiye zama. Mimi ndiye hufanya upya michana na nyusiku na ndiye huwaleta wafalme hawa baada ya wengine.” Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh.” (Fath-ul-Baariy (10/565)).

Faida!

´Allaamah Ibn-ul-Qayyim amesema:

”Kutukana zama kunazungukia katika mambo mawili ni lazima kupatikane moja kati ya mambo hayo mawili:

1 – Ima kufanya hivo ni kumtukana Allaah.

2 – Kumshirikisha.

Akiamini kuwa Allaah pekee ndiye ambaye amefanya hivo na hivyo akamtukana aliyefanya hivo basi anakuwa amemtukana Allaah.” (Zaad-ul-Ma´aad (02/355)).

[3] al-Bukhaariy (7491) na Muslim (2246).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 21-22
  • Imechapishwa: 05/10/2022