Kabla ya kuingia ndani msingi wa kitabu ningependa kutanguliza kanuni muhimu zinazohusiana na majina na sifa za Allaah[1].

1 – Ulazima wa maandiko ya Qur-aan na Sunnah inapokuja katika majina na sifa za Allaah

Ni lazima maandiko ya Qur-aan na Sunnah kuyabakiza yale majulisho yake katika uinje wake pasi na kubadilisha. Allaah ameiteremsha Qur-aan kwa lugha ya kitabu cha wazi. Isitoshe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anazungumza lugha ya kiarabu. Kwa hiyo ikalazimika kuyabakiza majulisho ya maneno ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama yalivyo kwa lugha hiyo. Kuyabadilisha kinyume na uinje wake ni kumsemea Allaah pasi na elimu, kitu ambacho ni haramu. Amesema (Ta´ala):

قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ

“Sema: “Hakika si vyenginevyo Mola wangu ameharamisha machafu, yaliyodhihirika na yaliyofichika na dhambi [aina zote] na ukandamizaji bila ya haki na [ameharamisha] kumshirikisha Allaah kwa ambayo hakukiteremshia mamlaka na kuzungumza juu ya Allaah yale ambayo hamyajui.”[2]

Mfano wake ni maneno Yake (Ta´ala):

بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ

“Bali mikono Yake imefumbuliwa… “[3]

Udhahiri wa Aayah mbili ni kwamba Allaah ana mikono miwili ya kweli. Kwa hiyo ni lazima kuthibitisha jambo hilo. Akisema mtu kuwa makusudio ya mikono ni nguvu tutamjibu kwa kumwambia kuwa huko ni kuyageuza maneno kutoka katika uinje wake, jambo ambalo halijuzu kwa sababu ni kumsemea Allaah pasi na elimu.

[1] Shaykh Muhammad Swaalih al-´Uthaymiyn ana kitabu kizuri kinachozungumzia majina na sifa za Allaah. Ametaja kanuni kadhaa muhimu kuhusu mada hii.

[2] 07:33

[3] 05:64

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 20
  • Imechapishwa: 05/10/2022