Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

وعن أنس رضي الله عنه قَالَ : مَرَّ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم بامرأةٍ تَبكي عِنْدَ قَبْرٍ، فَقَالَ : (اتّقِي الله واصْبِري) فَقَالَتْ: إِليْكَ عَنِّي؛ فإِنَّكَ لم تُصَبْ بمُصِيبَتي وَلَمْ تَعرِفْهُ، فَقيلَ لَهَا : إنَّه النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم فَأَتَتْ بَابَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم، فَلَمْ تَجِدْ عِنْدَهُ بَوَّابينَ، فقالتْ: لَمْ أعْرِفكَ، فَقَالَ: (إنَّمَا الصَّبْرُ عِنْدَ الصَّدْمَةِ الأُولى). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

.وفي رواية لمسلم: (تبكي عَلَى صَبيٍّ لَهَا)

31 – Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpitia mwanamke ambaye alikuwa analia kwenye kaburi na kumwambia: “Mche Allaah na kuwa na subira!” Akasema: “Niondokee, hujafikwa na msiba ulonifika!” [na mwanamke huyo] hakumtambua [aliyemwambia vile].  Akaambiwa: “Huyo alikuwa ni Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akaenda mpaka kwenye mlango wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na hakukua walinzi. Akamwambia: “Sikukutambua.” Akasema: “Hakika mambo yalivyo subira wakati wake ni pale mwanzoni mwa kupatwa na msiba.”[1]

Subira ambayo mtu anapewa thawabu kwayo ni ile inayokuwa wakati wa mwanzo. Wakati huu ndio mtu anatakiwa kuwa na subira na huku akitaraji malipo kwa Allaah. Wakati huohuo atambue kuwa ni Chake Allaah kile alichokichukua kama ambavyo ni Chake alichokuwa amempa. Atambue kuwa kila kitu kina muda wake maalum uliyopangwa.

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/229)
  • Imechapishwa: 26/02/2023