Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

وعن أنس رضي الله عنه قَالَ: مَرَّ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم بامرأةٍ تَبكي عِنْدَ قَبْرٍ، فَقَالَ: (اتّقِي الله واصْبِري) فَقَالَتْ: إِليْكَ عَنِّي؛ فإِنَّكَ لم تُصَبْ بمُصِيبَتي وَلَمْ تَعرِفْهُ، فَقيلَ لَهَا: إنَّه النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم فَأَتَتْ بَابَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم، فَلَمْ تَجِدْ عِنْدَهُ بَوَّابينَ، فقالتْ: لَمْ أعْرِفكَ، فَقَالَ: (إنَّمَا الصَّبْرُ عِنْدَ الصَّدْمَةِ الأُولى). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

.وفي رواية لمسلم: (تبكي عَلَى صَبيٍّ لَهَا)

31 – Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpitia mwanamke ambaye alikuwa analia kwenye kaburi na kumwambia: “Mche Allaah na kuwa na subira!” Akasema: “Niondokee, hujafikwa na msiba ulonifika!” [na mwanamke huyo] hakumtambua [aliyemwambia vile].  Akaambiwa: “Huyo alikuwa ni Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akaenda mpaka kwenye mlango wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na hakukua walinzi. Akamwambia: “Sikukutambua.” Akasema: “Hakika mambo yalivyo subira wakati wake ni pale mwanzoni mwa kupatwa na msiba.”[1]

Miongoni mwa faida ya Hadiyth hii ni pamoja na kwamba kulia mbele ya kaburi kunapingana na kuwa na subira. Kwa ajili hii ndio maana amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mche Allaah na kuwa na subira.”

Kuna watu wenye kupewa mtihani. Anapokufa maiti anakuwa ni mwenye kuliendea kaburi mara kwa mara na kulia mbele yake. Tendo hili linapingana na kuwa na subira. Badala yake tunasema ikiwa unataka kumnufaisha maiti huu muombee ilihali uko nyumbani kwako. Hakuna haja ya kulienda kaburi mara kwa mara kwa sababu jambo hili linamfanya mtu kumfikiria [kumuwaza] maiti huyu siku zote na hambanduki akilini. Jambo hili linamfanya kutoweza kusahau msiba. Kinyume chake lililo bora mtu anatakiwa kuusahau na kuufuta msiba kiasi na anavoweza.

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/229)
  • Imechapishwa: 26/02/2023