Swali: Hizbiy akinialika niitikie mwaliko wake? Akizungumzia kitu kuhusu Hizbiyyah nitamraddi na asipozungumzia kitu kuhusu Hizbiyyah sintomzungumzia. Je, niitikie mwaliko wake au hapana?

Jibu: Ikiwa ni mwaliko wa harusi na una uhakika kuwa hakutotokea maovu wala mawaidha, basi hapana vibaya ukaenda na ukala chakula.

Lakini ikiwa unajua kuwa watawalingania watu katika Hizbiyyah au watawakimbiza watu mbali na Ahl-us-Sunnah na kusema kuwa ”Ni kweli kwamba ni mwanachuoni, lakini hana uelewa. Ni kweli kwamba ni mwanachuoni, lakini ana msimamo mkali. Ni kweli kwamba ni mwanachuoni, lakini anamili katika Takfiyr na kadhalika”, inatakiwa kuepuka vikao kama hivi vya batili.

Kuhusu mawaidha na mikusanyiko yao ya ki-Da´wah, mimi nawanasihi ndugu kutovihudhuria. Wameshughulishwa. Hawana muda. Isipokuwa tu muda wa kufanya uchaguzi. Vinginevyo wameshughulishwa. Kwa nini? Kwa porojo na kuwatafuta wafanya biashara kana kwamba ni watumishi wao.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=26 Tarehe: 1418-03-23/1997-07-28
  • Imechapishwa: 05/11/2022