Kama tulivosema anayefuata njia ya wale walioneemeshwa atapewa mtihani, atabanwa, atatwezwa, atazingatiwa kuwa ni mpotofu na kutishwa. Kwa hivyo anatakiwa kuwa na subira. Imetajwa katika Hadiyth ya kuwa katika zama za mwisho mtu ambaye atashikamana na dini ni kama ambaye anashika kaa la moto. Kwa sababu atakutana na maudhi na shari kutoka kwa watu. Kwa hiyo anahitaji kufanya subira kama ambaye ameshika kaa la moto. Si kama kucheza kwenye waridi. Kazi ina matatizo na maudhi kutoka kwa watu. Kwa hiyo anahitaji kuwa na subira na thabati mpaka utapokutana na Mola wako (´Azza wa Jall) ukiwa na hali hiyo ili uweze kusalimika kutokamana na Moto. Utasalimika na upotofu duniani na Aakhirah utasalimika kutokamana na Moto. Hakuna njia nyingine isipokuwa hii. Hakuna njia ya uokozi isipokuwa kushika njia hii.

Hii leo wanakoseshwa nusura mfumo wa Salaf katika magazeti, majarida na vitabu. Wanawatweza Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na wale Salafiyyuun wa kikweli. Wanasema kuwa wana msimamo mkali na kwamba ni Takfiyriyyuun na haya na yale – lakini haya hayadhuru. Lakini haya yanamuathiri mtu ambaye hana subira na hana azma yenye nguvu. Yanaweza kumuathiri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mf04-01-1435.mp3
  • Imechapishwa: 05/11/2022