Swali: Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika yeye [ad-Dajjaal] ni chongo na hakika Mola wenu sio chongo.”

Je, kumethibitishwa macho mawili kwa Allaah?

Jibu: Ndio, kumethibitishwa macho mawili. Adiha kusikia na kuona zimetajwa ndani ya Qur-aan tukufu.

Swali: Ni kwa njia ya kipimo?

Jibu: Hapana, ni dalili ya wazi:

“… sio chongo.”

maana yake ni kwamba Mola wako ana macho mawili. ad-Dajjaal ana jicho moja na jicho jengine limefutika. Mola wako ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona, mpole, Mwenye huruma, anaghadhibika, anaridhika, anatoa na anazuia (´Azza wa Jall):

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.”[1]

[1] 42:11

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22664/هل-في-حديث-ليس-باعور-اثبات-العينين-لله
  • Imechapishwa: 15/07/2023