Kuacha kutahiriwa si ni kujifananisha na makafiri?

Swali: Je, mtu anaweza kusema kuwa kutahiriwa ni wajibu?

Jibu: Haya ndio maoni ya kikosi kikubwa cha wanazuoni. Kwa sababu imepokelewa katika baadhi ya Hadiyth. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema wakati waliposilimu baadhi ya makafiri:

“Jiondoshe kikoi cha ukafiri na utahiri.”

Lakini kilichotangaa ni kwamba inapendeza. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwaamrisha watu wote wafanye jando. Kwa hiyo ikafahamisha kuwa ni jambo la kupendeza.

Swali: Je, mtu akiacha kutahiri si anakuwa amejifananisha na washirikina?

Jibu: Hapana, sio kujifananisha. Wako washirikina wanaofanya jando wakiwemo mayahudi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22657/ما-الصحيح-في-حكم-الختان
  • Imechapishwa: 15/07/2023