Ndoa ya kustarehesha (المسيار) ni mwelekeo mpya ambao hautimizi malengo ya ndoa isipokuwa tu jimaa; mwanaume hamtunzi mwanamke, hamhudumii mwanamke, hamsimamii mwanamke. Hili limezuka pale ambapo wanawake wameanza kufanya kazi na wala hataki kumtegemea mume. Ni jambo limezuka. Sio ndoa iliyokamilika. Ni kweli kwamba ni halali lakini bado si kamilifu kwa sababu haitimizi malengo ya ndoa; hamsimamii mwanamke, hamlindi. Kazi ni yeye kutoka na kurudi na kutimiza matamanio yake. Ni jambo lisilokuwa la sawa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (41)
  • Imechapishwa: 05/10/2023