Swali: Kuna uwezekano kukaweko kujivua (الخلع) bila fidia?

Jibu: Hapana, hakuna kujivua pasi na fidia.

Swali: Lakini vipi ikiwa mume hataki kitu?

Jibu: Hivyo inahesabika kama talaka na si kujivua. Katika hali hiyo anaweza pia kumrejea.

Swali: Hata hivyo hawezi kumrejea wakati wa eda yake baada ya kujivua kwake?

Jibu: Hapana, hawezi kumrejea. Lazima wafunge ndoa upya. Ikiwa wameachana kwa fidia, basi ni lazima wafunge ndoa upya.

Swali: Na ni lazima waote wawili wakubaliane?

Jibu: Ndio.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22284/هل-يصح-الخلع-بين-الزوجين-بدون-مال
  • Imechapishwa: 03/10/2022