Swali: Kunyoa nywele zote za kichwani katika msimu usiokuwa wa hajj ni katika mwenendo wa Khawaarij?

Jibu: Hapana vibaya akizinyoa na akaona manufaa ya kufanya hivo. Khawaarij wanawalazimisha wafuasi wao kunyoa. Ni katika alama zao. Msingi wa jambo inafaa kwa mujibu wa Shari´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinyoa kipara katika hajj ya kuaga na akapunguza nywele katika ´umrah. Wakati usiokuwa wa hajj na ´umrah inafaa kufanya hivo. Hilo ni kama alivosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Ima nyoa zote au ziache zote.”[1]

[1] al-Muhallaa (7/211).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21939/حكم-حلق-الراس-كاملا-في-غير-النسك
  • Imechapishwa: 03/10/2022