25. Kitu cha sita kinachomsaidia mwanamke kuwa mwema

6 – Miongoni mwa mambo yatayomfanyia wepesi mwanamke kupata tabia njema ni yeye kuchagua mume mwema na msichana pale mwanzoni kabisa asimkubali isipokuwa yule ambaye yuko na tabia na dini ambaye atamsaidia juu ya jambo la Aakhirah. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atapokujieni yule ambaye mmeridhia kwake tabia na dini yake basi muozesheni. Msipofanya hivo basi kutakuwa na fitina katika ardhi na ufisadi mkubwa.”[1]

[1] at-Tirmidhiy (1084), Ibn Maajah (1967) na wengineo. Ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (03/20).

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Shuwmaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 42-43
  • Imechapishwa: 03/10/2022