24. Kitu cha tano kinachomsaidia mwanamke kuwa mwema

5 – Miongoni mwa mambo makubwa yanayomsaidia mke juu ya wema wake ni kutangamana na wanawake wema na wenye kumcha Allaah na kusikiliza maneno yao, kujitahidi kujifananisha nao. Sambamba na hilo ajiepushe kutangamana na wanawake waovu na kutoketi nao wala kuwasikiliza. Bali awe na tahadhari kwelikweli kuangalia wale wanawake wenye kuonyesha mapambo na walio uchi. Ni mamoja anafanya hivo kupitia TV, video au njia zingine. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mfano wa rafiki mzuri na rafiki muovu ni kama muuza manukato na muhunzi. Muuza manukato ima atakupa au utapata kutoka kwake harufu nzuri. Kuhusu muhunzi ima ataunguza nguo yako au utapata harufu mbaya kutoka kwake.”[1]

an-Nawawiy amesema.

“Ndani yake kuna ubora wa kukaa na watu wema, watu wa kheri, wenye heshima, wenye tabia njema, wenye kujichunga, wanazuoni, watu wa adabu na makatazo ya kukaa na watu waovu, Ahl-ul-Bid´ah, wenye kuwasengenya watu, amekithirisha uovu wake na kutokuwa kwake na kazi na mfano wa hao katika aina nyenginezo zilizokuwa mbaya.”[2]

ar-Raaghib amsema:

“Amezindua katika Hadiyth hii ya kwamba ni haki kwa mtu kujitahidi kwa kiasi cha ijitihada yake kutangamana na kukaa na watu wa kheri. Kwani jambo hilo linaweza kumfanya mtu ambaye ni muovu akawa mwema kama ambavo kusuhubiana na waovu kunaweza kumfanya aliye mwema akawa muovu.

Ni kitu kinachotambulika kuwa maji na upepo hubadilika na kuharibika wakati vinapokaribiana na mzoga. Tusemeje kuhusu nafsi za watu ambazo hukubali zaidi kile ambacho kinawekwa ndan yake ni mamoja iwe ni kheri au shari?”[3]

[1] al-Bukhaariy (04/323) na (09/660 – Fath), Muslim (2628) na wengineo.

[2] Sharh Muslim (16/178).

[3] Imenakiliwa kutoka katika ”Fawdhw-ul-Qadiyr” (05/507).

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Shuwmaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 40-42
  • Imechapishwa: 03/10/2022