23. Kitu cha nne kinachomsaidia mwanamke kuwa mwema

4 – Kumtaka msaada Allaah (Ta´ala). Hakika mtu hawezi kufikia katika kheri yoyote iliyo ndogo kabisa isipokuwa kwa hifadhi ya Allaah (Ta´ala), tawfiyq Yake, msaada Wake na kumfanya Kwake mtu kuwa imara. Amesema (Tabaarak Ismuh) kuhusu haya:

فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّـهُ

“Basi wanawake wema ni wale watiifu wenye kujihifadhi katika hali ya kutokuweko waume zao kwa kuwa Allaah ameamrisha wajihifadhi.”[1]

Maneno Yake (Ta´ala):

بِمَا حَفِظَ اللَّـهُ

“… kwa kuwa Allaah ameamrisha wajihifadhi.”

Bi maana kwa Allaah kuwahifadhi ndipo wakawa hivyo. Hivyo ndivo alivosema at-Twabariy[2] na kikosi cha wafasiri wa Qur-aan.

[1] 04:24

[2] Jaamiy´-ul-Bayaan (05/39).

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Shuwmaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 40
  • Imechapishwa: 03/10/2022