Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

124 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

يَا نِسَاءَ المُسْلِمَاتِ، لا تَحْقِرنَّ جَارَةٌ لِجَارَتِهَا وَلَوْ فِرْسِنَ شاةٍ

“Enyi wanawake waislamu! Jirani asidharau kumpa zawadi jirani mwenzake japo kwato ya mbuzi.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Katika Hadiyth hii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anahimiza jirani kumpa jirani mwenzake zawadi ijapo kama itakuwa kitu kidogo. Kana kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anataka kusema mtu asidharau mema hata kama itakuwa kitu kidogo tu. Imethibiti ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Utapopika mchuzi basi weka maji mengi na umpe jirani yako.”[1]

Hata mchuzi ukimpa jirani kama zawadi unapewa thawabu kwa hilo. Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Usidharau chochote katika wema hata kama ni kumtazama ndugu yako kwa uso wenye bashasha.”

Hakika hili ni katika wema pia. Ukikutana na ndugu yako na uso wenye bashasha, hili pia ni katika kheri na mema. Kwa sababu ukikutana na ndugu yako namna hii anaingiwa na furaha. Kila chenye kumfanya ndugu yako muislamu akafurahi, basi ni kheri na thawabu. Kila chenye kumfanya kafiri akakasirika, vilevile ni kheri na thawabu. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَا يَطَئُونَ مَوْطِئًا يَغِيظُ الْكُفَّارَ وَلَا يَنَالُونَ مِنْ عَدُوٍّ نَّيْلًا إِلَّا كُتِبَ لَهُم بِهِ عَمَلٌ صَالِحٌ

“… na wala hawakanyagi njia inayowaghadhibisha makafiri na wala hawawasibu maadui msiba wowote isipokuwa wanaadikiwa kwayo tendo jema.” (09:120)

[1]Muslim (2625).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/168-169)
  • Imechapishwa: 30/04/2024