Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

وعن أبي هريرة – رضي الله عنه – قال: قال رسول الله صلي الله عليه وسلم ((صلاة الرجل في جماعة تزيد على صلاته في بيته وصلاته في سوقه بضعاً وعشرين درجة، وذلك أن أحدهم إذا توضأ فأحسن الوضوء، ثم أتي المسجد لا ينهزه إلا الصلاة، لا يريد إلا الصلاة، فلم يخط خطوة إلارفع له بها درجة، وحط عنه بها خطيئة حتى يدخل المسجد، فإذا دخل المسجد كان في الصلاة، ما كانت الصلاة هي تحبسه، والملائكة يصلون على أحدكم ما دام في مجلسه الذي صلي فيه يقولون: اللهم ارحمه، اللهم اغفر له، اللهم تب عليه، ما لم يؤذ فيه، ما لم يحدث فيه) (متفق عليه)

10 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimuliaya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mtu kuswali na mkusanyiko huzidi kuswali sokoni au nyumbani kwake kwa daraja zaidi ya ishirini na saba. Hilo ni kwa mmoja wao anapotawadha vizuri na kisha akaenda msikitini na hakuna jengine lililomuinua isipokuwa swalah. Kwa hiyo hatopiga hatua atainuliwa daraja kwa hatua hiyo na atafutiwa dhambi kwa daraja hiyo mpaka pale atapoingia msikitini. Atapoingia msikitini atakuwa yuko bado katika swalah muda wa kuwa swalah ndio imemzuia. Malaika humwombea rehema mmoja kati yenu midhali yuko katika kikao chake alichoswalia kwa kusema: “Ee Allaah! Mrehemu”, “Ee Allaah! Msamehe”, “Ee Allaah! Mkubalie tawbah yake”. Huendelea hivo maadamu hajaudhi wala hajapata hadathi.”[1]

Nukta muhimu katika Hadiyth hii ni “kisha akaenda msikitini na hakuna jengine lililomuinua isipokuwa swalah.” Ni dalili inayoonyesha inatakiwa kwa mtu kuhudhurisha nia ili aweze kupata ujira huu mkubwa.

Ama kwa mfano atatoka nyumbani na hakusudii kwenda kuswali, haandikiwi ujira huu. Kwa mfano mtu atoke nyumbani kwake na kwenda dukani kwake na walipoadhini akaenda kuswali. Katika hali hii hapati ujira huu. Ujira huu unahusu yule mwenye kutoka nyumbani kwake na hakuna kilichomtoa isipokuwa ni swalah.

Huenda akaandikiwa ujira huu kutokea pale anapotoka dukani kwake au sehemu ya biashara yake mpaka kufika kwake msikitini maadamu ametoka sehemu hii ilihali yuko na wudhuu’.

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/74)
  • Imechapishwa: 30/01/2023