Fadhilah kwa mtu ambaye wakati fulani anaacha swalah zinazopendeza

Swali: Je, mtu anapata fadhilah zilizotajwa akihisi uvivu kuswali Sunnah Rak´ah nne kabla ya Dhuhr na Rak´ah nne baada ya Dhuhr?

Jibu: Ni swalah inayopendeza na hakuna juu yake kitu. Ni swalah inayopendeza na hapati dhambi.

Swali: Je, anapata fadhilah hizi ya kwamba ataingia Peponi?

Jibu: Pepo imefungamana na kufanya yale aliyowajibisha Allaah na kuyaacha yale aliyoharamisha. Muumini ameahidiwa Pepo ijapo hatoswali swalah zinazopendeza. Lakini akiswali swalah zinazopendeza ngazi yake inakuwa ya juu zaidi kuliko zilizotangulia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22555/هل-يحصل-فضل-سنن-الظهر-لو-تركها-احيانا
  • Imechapishwa: 16/06/2023