Swali: Nimekusikia mara nyingi ukisema kuwa ambaye anakusudia kuchelewesha swalah ya Fajr anakuwa kafiri. Kujengea juu ya hili akifungisha ndoa ilihali haswali Fajr ndoa inasihi?

Jibu: Wanazuoni wamekinzana. Kikosi cha wanazuoni wengi wanaona kuwa hakufuru muda wa kuwa hajapinga uwajibu wake. Wanaona kuwa anakufuru kufuru ndogo. Maoni sahihi ni kwamba anakufuru kufuru kubwa akikusudia kuacha swalah kwa makusudi mpaka ukatoka wakati wake pasi na kuwepo kikwazo. Katika hali hiyo kafiri hamfungishi ndoa mwanamke wa Kiislamu. Ikiwa walii wake haswali basi atafute walii mwingine. Ambaye haswali hatakiwi kusimamia ndoa yake. Baba ambaye haswali, basi amfungishe ndoa mwingine kama vile mwanawe wa kiume au ami yake. Mtu wa karibu na karibu zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22545/هل-يصح-زواج-وعقد-من-لا-يصلي-الفجر
  • Imechapishwa: 16/06/2023