Swalah ya Sunnah Rak´ah nne kwa Tasliym moja inasihi?

Swali: Kuswali swalah ya Rak´ah nne kwa Tasliym moja.

Jibu: Haitakikani. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah ya usiku na mchana ni [Rak´ah] mbilimbili.”

Haya yamekuja kama maamrisho.

Swali: Je, swalah ni sahihi?

Jibu: Ni sahihi – Allaah akitaka. Kwa sababu kuna jopo la wanazuoni waliosema hivo. Baadhi ya mapokezi yanaweza kuashiria hivo. Lakini Sunnah ni mtu achunge Rak´ah mbilimbili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22554/حكم-صلاة-النافلة-الرباعية-بتسليمة-واحدة
  • Imechapishwa: 16/06/2023