Dalili ya unajisi wa damu na swalah ya aliyeumia

Swali: Ni ipi dalili juu ya unajisi wa damu?

Jibu: Kule Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuamrisha kuiosha. Baadhi wamesimulia kwamba kuna maafikiano ya wanazuoni juu ya kwamba ni najisi. Isipokuwa damu kidogo inasamehewa. Damu ndogo isiyotoka katika tupu ya mbele wala tupu ya nyuma – kwa mfano damu inayotoka kwenye meno, macho au puani na ikawa ni ndogo – inasamehewa.

Swali: Vipi kuhusu ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) kuswali na damu?

Jibu: Aliyeumia na mwanamke mwenye damu ya ugonjwa wanasamehewa. Wanaswali kutegemea na hali zao. Ambaye ameumua anatembea anaswali kutegemea na hali yake:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Basi mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

[1] 64:16

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22546/ما-دليل-نجاسة-الدم-وحكم-صلاة-المجروح
  • Imechapishwa: 16/06/2023