Pindi adhaana ya muadhini inasikika mji mzima

Swali: Je, adhaana ni faradhi yenye kutosheleza kwa mkusanyiko au kwa watu wote wa mji?

Jibu: Ni faradhi yenye kutosheleza kwa kila upande muda wa kuwa hawasikii adhaana ya mwengine. Kila upande walipo na msikiti ni faradhi yenye kutosheleza kwao. Lakini ikiwa muadhini anawasikilizisha watu wote itatosha. Katika hali hiyo kwa wengine itakuwa ni jambo linalopendeza. Ikiwa muadhini ana sauti ya kuweza kuwasikilizisha watu wote basi kwa wengine itakuwa inapendeza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22547/هل-الاذان-فرض-على-كل-بلد-ام-كل-مسجد
  • Imechapishwa: 16/06/2023