08. Matonge kumi na moja kwa siku

30 – Sa´iyd bin Sulaymaan ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdul-Hamiyd bin Sulaymaan, kutoka kwa Abu Haazim, ambaye amesema:

”Nilisema kumuuliza Sahl bin Sa´d: ”Je, uliona vinu vya unga wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?” Akasema: ”Sikuona vinu vya unga kipindi hicho. Hakuna kitu alichosagiwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwezi mmoja mpaka alipoiaga dunia.” Nikasema: ”Sasa mlikuwa mnafanya nini?” Akasema: ”Tulikuwa tunasaga. Kisha tunapuliza maganda yake. Kisha kinaruka kinachoruka, na kinabaki kinachobaki.”

31 – al-Qaasim bin Muhammad bin Ibraahiym al-´Absiy ametuhadithia: Hushaym bin Swaaswaan ametuhadithia, kutoka kwa ´Ubaydullaah bin ´Umar, kutoka kwa Naafiy´, kutoka kwa Ibn ´Umar, ambaye ameeleza:

”Alikuwa anahudhuria chakula cha ´Umar. Kila siku alikuwa anachukua matonge kumi na moja, ambayo anayagawa atakavyo kwa ajili ya siku inayofuata.”

32 – ´Ubayd bin Muhammad amenihadithia: Abu Usaamah ametuhadithia: Sulaymaan bin al-Mughiyrah ametuhadithia, kutoka kwa Thaabit, ambaye amesema:

”´Umar bin al-Khattwaab alitamani kinywaji, akaletewa kinywaji cha asali. Akawa anakizungusha chombo mkononi mwake na kusema: ”Ukikinywa, utaondoka utamu wake na kubakia uchungu wake.” Baada ya hapo akampokeza mtu mwingine akakinywa.”

33 – ´Aliy bin Muslim bin Sa´iyd ametuhadithia: ´Abbaad bin ´Abbaad ametuhadithia, kutoka kwa Ja´far bin az-Zubayr, kutoka kwa al-Qaasim bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Abu Umaamah, ambaye amesema:

”´Aliy (Rahimahu Allaah) alipewa bata aliyejazwa tende na siagi. ´Aliy akasema: ”Hii ndio sababu ya Quraysh kuuana.”

34 – Muhammad bin Ahmad al-Qurashiy amenihadithia, kutoka kwa Muhammad bin Ziyaad, kutoka kwa Zabbaan al-Kulaybiy, kutoka kwa baba yake, aliyesema:

”Wakati Musw´ab bin az-Zubayr alipomuua al-Mukhtar, ´Amr bin Hurayth alimtengenezea chakula. Akala yeye pamoja na wenzake. Kisha akamhudumia Faaluudhajah[1], iliyobubujika kwenye sahani. Musw´ab akawaambia wenzake: ”Njooni mle. Naapa kwa Allaah! Dini haijapatapo kuhusiana na watoto wa ngamia [tupu] na kamwe haitokuwa hivo. Vita havijatokana na kitu kingine isipokuwa yale mnayoyaona na pakiti za wanyama wanaopandwa.”

[1] Tamtam iliyotengenezwa kwa maziwa, maji na asali.

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 46-49
  • Imechapishwa: 14/06/2023