Du´aa unapomuona aliyepewa mtihani ndani ya swalah

Swali: Mtu anapomuona aliyepewa majaribio ilihali anaswali amwombe Allaah amwondoshee mtihani ilihali yuko ndani ya swalah? Je, aseme:

الْحَمْدُ الله الَّذِي عافاني مِمَّا ابْتَلاك به وفَضَّلني على كَثِيرٍ مِمَّنْ خَلَقَ تَفْضِيلاً

“Himdi zote ni Zake Allaah ambaye Ameniepusha na kile Alichokupa mtihani na Akanifanya mimi kuwa bora kuliko wengi miongoni mwa Aliowaumba?”

 Jibu: Hakuna vibaya. Akiwa kwenye Sujuud au mwishoni mwa swalah hapana vibaya ikiwa ni du´aa ya kwenye Sujuud, mwishoni mwa swalah kabla ya kutoa salamu na kwenye Qunuut.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23139/هل-يقال-دعاء-من-راى-مبتلى-في-الصلاة
  • Imechapishwa: 11/11/2023