Du´aa ya kumuomba Allaah yale yanayopelekea katika rehema Zake

Swali: Ni upi usahihi wa du´aa inayosema:

أسألك موجبات رحمتك

“Nakuomba yale yanayopelekea katika rehema Zako… ?”

Ibn Baaz: Sijarejelea cheni yake ya wapokezi. Wewe uko na maelezo yake ya chini?

Mwanafunzi: Ndio. Katika cheni yake yumo Humayd al-A´raaj. adh-Dhahabiy amesema katika “al-Miyzaan”:

“Ni mwenye kuachwa.”

Ahmad amesema:

“Dhaifu.”

Abu Zur´ah amesema:

“Mnyonge.”

ad-Daaraqutwniy amesema:

“Ni mwenye kuachwa.”

Ibn Baaz: Ni du´aa nzuri hata kama haikupokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23141/ما-صحة-حديث-اسالك-موجبات-رحمتك
  • Imechapishwa: 11/11/2023